Katika jitihada za kuimarisha usalama wa shule na jamii, tulipata ugeni wa kipekee kutoka kwa maafisa wa polisi waliobobea katika huduma za kuzima moto. Wanafunzi pamoja na walimu (staff) walifundishwa kwa vitendo namna ya kuchukua tahadhari wakati wa moto, kutumia vifaa vya kuzimia moto kwa usahihi, na njia sahihi za kujiokoa na kusaidiana kwa usalama.
Mafunzo haya si tu yanawajengea wanafunzi uelewa wa hali halisi ya dharura, bali pia yanawawezesha walimu kuwa mstari wa mbele katika kulinda maisha ya watoto na wafanyakazi wenzao. Elimu hii ni nguzo muhimu kwa usalama wa shule na jamii nzima.
Comments are closed, but trackbacks and pingbacks are open.